Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

USILETE UTANI KATIKA MAPENZI

USILETE UTANI KATIKA MAPENZI

Mdada mmoja alitaka kujua kiasi gani anapendwa
na mume wake, hivyo akataka kujua mumewe
atafanya nini endapo ataamua kuondoka na
kumuacha!
Mwanamke huyo akaamua kuandika barua
inayosema "Samahani mume wangu, nimeamua
kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya mbali
na wewe"Barua hiyo akaiweka juu ya meza iliyokuwa
chumbani.

Baadaye jioni, muda wa Mumewe kurudi
mwanamke huyo akajificha chini ya uvunguni wa
wakitanda mule chumbani Mume alipoingia
chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma
kisha, akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua,
halafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku
akipiga milunzi na akiwa anavua nguo.Akapiga simu
na akasikika akisema hivi "hello mpenzi, nina raha
sana leo.. yule mwanamke nuksi ameondoka mwenyewe bila kumfukuza
nakutuachia uwanja, jiandae
nakuja"Muda huo huo Mume akaondoka.
Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa analia na kutokwa na machozi akaamua kutoka
lakini amenyong'onyea na amelowa mashavu kwa
machozi.
Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua
mumewe aliandika kitu gani kwenye ile barua.
Akakuta maneno haya "nimekuona miguu yako
uvunguni tafadhali andaa chakula nina njaa sana
mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa
nilisahau kupitia. Nakupenda mke wangu
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright HOT STORIES AND NEWS
Back To Top